Tumaini la KrismasiMfano
Je, huna muda wa Yesu?
Soma Luka 2:7.
Kuna mwaka watoto wetu wakiwa bado wachanga, mke wangu aliamua kuwa ni mimi nitachangua wapi tutaenda likizo kama familia. Niliamua nilitaka kufanya likizo huria kabisa bila ya mipango yoyote. Kama mchungaji na kiongozi, kila siku ya maisha yangu imepangwa. Kupanga likizo sio jambo rahisi!
Likizo ya kighafla kabisa wakati tayari uko katika ndoa na watoto sio wazo zuri. Bila ya kufanya mipango yoyote ya usiku tano za kwanza za likizo hiyo katika miji mitano tofauti, tulilala katika gari letu usiku nne kati ya hizo tano kwa sababu hatukuweza pata gesti au hoteli iliyokuwa na nafasi. Watoto wangu hawakuwa wanakambi wenye furaha. Usiku wa tano, tuliamua kufanya mipango.
Likizo hiyo ilinisaidia kuelewa kile Biblia huwa inamaanisha wakati tunaambiwa katika hadithi ya Krismasi ya Kwanza kuwa hakukuwa na gesti yoyote kwa Maria na Yusufu.
Ujio wa Mungu wa milele na Masihi aliyetabiriwa ulikuwa umetarajiwa kwa maelfu ya miaka. Unabii ulitabiri ukweli kuwa Mwokozi wa dunia atakuja. Kuzaliwa kwake kungekuwa kwa maana sana hadi kungegawanya historia katika B.C. (Kabla Kristo Kuzaliwa) na A.D. (Baada ya Kifo cha Kristo). Siku yako ya kuzaliwa imepewa tarehe kulingana na siku ya kuzaliwa ya Yesu.
Ilhali, wakati Mwana wa Mungu alikuja duniani, hakukuwa na nafasi ya chumba kwa ajili yake. Mwenye vyumba alikosa fursa kuu. Kama Yesu angezaliwa katika moja wapo wa vyumba vyake, mwenye vyumba angejenga ishara kubwa inayosoma, "Mwana wa Mungu Amezaliwa Hapa!" Angelipisha bei ghali kwa sababu ya vyumba vyake! Badala yake, alipoteza baraka kubwa sana ya maisha yake kwa sababu hakuwa na chumba kwa ajili ya Yesu.
Hatuwezi tukamulaumu mwenye vyumba kwa ajili ya kukosa chumba cha Yesu. Huwa tunafanya hivyo kila wakati.
Huwa tunapinga kumpatia umuhimu anaostahili maishani mwetu. Tunajaza ratiba yetu na matukio ambayo hayana maana tukilinganisha na Yesu. Tunatumia pesa zetu kwa kununua vidude vipya na hatuna chochote cha kumpa Mungu kwa kazi yake ulimwenguni. Tunatumia muda wetu wote kuendeleza kazi zetu ilhali tunasema hatuna muda wa kuwasaidia wengine katika kanisa letu na jamii.
Unapojitayarisha kusherehekea Krismasi mwaka huu, jiulize swali hili: Je umemuachia Yesu chumba katika gesti yako?

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.
More
Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa