Tumaini la KrismasiMfano
Orodha ya Krismasi ya Yesu
Soma mistari ya leo ya Biblia.
Kwa zaidi ya miaka 50 familia yangu imekuwa na utamaduni wa kuwa na sherehe ya kuzaliwa kwa Yesu. Ilianza nilipokuwa na umri wa miaka 3 na nikauliza mama yangu, "Krismasi ni nini?" Mamangu aliniambia ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Yesu. Nikiwa na wazo kali la mtoto wa miaka 3, nilisema, "Inafaa tuwe na sherehe ya kuzaliwa!" Na tulikuwa nayo, kamili na keki ya siku ya kuzaliwa, vinywaji, nyimbo, keki na mishumaa.
Tumeendelea na utamaduni huo kwa vizazi vinne sasa. Sherehe ya kuzaliwa kwa Yesu imekuwa muda takatifu ambapo tunasoma hadithi ya Krismasi na kusema ni nini tunatolea shukrani na nini tunampatia Yesu, ambayo ni sehemu moja wapo ya kukumbukwa kwa sherehe hiyo.
Mara nyingi, Yesu husahaulika wakati wa Krismasi. Fikiria ya kuwa, nilikupangia sherehe na nikaalika watu wengi. Kila mtu alileta zawadi nyingi sana, na walioalikwa walibadilishana zawadi wao wenyewe — na wewe hukupata chochote.
Hiyo ndio Krismasi. Tunapatia kila mtu zawadi isipokuwa Yesu. Hembu tuambiane ukweli — ni nini utampea Mungu aliye na kila kitu?
Kwa kweli, Yesu hana kila kitu. Kuna vitu vinne ambavyo hana ila wewe umpe hii Krismasi:
Mpe tumaini yako. Imani ni suala la hiari. Yesu hana tumaini yako isipokuwa umpatie. Kamwe hatawai lazimisha chochote.
Mpe Yesu nafasi ya kwanza maishani mwako. Kama kuna kitu au mtu isipokuwa Yesu kinachochukua nafasi ya kwanza maishani mwako, ni sanamu. Krismasi hii, chagua kumfanya Yesu awe wa kwanza katika maisha yako ya kifedha, nia zako, mahusiano, ratiba — na hata katika matatizo yako.Mpe Yesu moyo wako. Moyo wako ndicho kitu unachokipenda, ndicho kitu unachokithamini na kitu unachokijali sana. Yesu anasema, "Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako" (Luka 12:34) Njia moja ya muhimu ya kumpa Yesu moyo wako Krismasi hii ni kwa kutoa rasilmali zako kwa kazi yake. Yesu haitaji pesa zako, lakini anataka kile kinachowakilishwa na pesa zako — moyo wako.
Walete watu wengine kwa Yesu. Mungu anataka Familia zaidi kuliko kitu kingine Krismasi hii. Anataka watoto wanaochagua kumpenda na kumtumainia. Ndio sababu kuu tunasherehekea Krismasi. Alika mtu kwa Yesu Krismasi hii. Ambia mtu kile ambacho Yesu amekutendea maishani mwako.
Biblia inatuambia kuwa Mamajusi hawakumpa Yesu mabaki wakati walipomtembelea Krismasi ya kwanza badala yake walimpea zawadi tatu muhimu za thamani: "Walimuinamia na kumuabudu. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: Dhahabu, Ubani na manemane" (Mathayo 2:11).
Unapompatia Yesu matumaini yako, mfanye awe wa kwanza maishani mwako, na uwalete watu wengine kwake, utakuwa unampatia zawadi zilizo na thamani sana kuliko zile ambazo Mamajusi walileta.
Kwa hivyo mpe Yesu "Furaha ya Kuzaliwa" Krismasi hii. Mpe kilicho bora zaidi.

Kuhusu Mpango huu
Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.
More
Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa