Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tumaini la KrismasiMfano

The Hope Of Christmas

SIKU 5 YA 10

Usimkose Yesu kazini

Soma Yohana 4:10.

Sasa hivi kuna mawimbi ya televisheni na redio yanakuzunguka. Ungekuwa na redio, ungeona kilicho kwenye mawimbi hayo. Kwa sababu huwezi yaona haimaanishi kuwa hayapo au si halisi. Hauko tu karibu na redio au televisheni.

Hivyo ndivyo kulikuwa Bethlehemu usiku wa Krismasi ya kwanza, Licha ya kuwa Bethlehemu ilikuwa na gesti yenye lengo la kuwashughulikia wasafiri, hakukuwa na chumba katika gesti kwa ajili ya familia muhimu sana ya wasafiri Bethlehemu usiku huo.

Krismasi hii, usikose usawa muhimu wa hadithi hii katika mioyo yetu wenyewe. Moyo wako uliumbwa kumshika Mungu. Uliumbwa na Mungu na wala sio kuumbwa wa Mungu. Hadi uelewe hayo, maisha kamwe hayatawai eleweka. Kwa bahati mbaya, tumejaza maisha yetu na mambo mengine. Tunawaalika wageni wengine manyumbani mwetu. Moyo wetu umejazwa na mawazo, nia, maadili, upendo na ahadi zingine.

Maisha yetu yamejaa hadi hatuna ufahamu wakati Yesu anatokea karibu nasi. Mungu hujitokeza katika maisha yetu kila mara, akitutolea fursa ambazo kamwe hatukudhani tungepata, katikati ya shida hatukujua tungepata. Lakini mara kwa mara huwa hatumuoni.

Haya yalitendeka kwa Biblia mara nyingi. Yesu angejitokeza na kuongea na watu ambao kamwe hawakutambua yeye ni nani. Katika kitabu cha Yohana, Yesu alikuwa amekaa karibu na kisima wakati mwanamke alimjia , akitafuta maji. Hakumtambua Yesu. Kwanza kiukweli, alianza mjadala wa kidini na Mwana wa Mungu! Kisha Yesu akasema, "Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekuambia, 'Nipatie maji ninywe,' ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yenye uhai." (Yohana 4:10) Lakini huyo mwanamke hakumtambua Yesu.

Mungu yuko kazini kote karibu nawe — sio tu wakati wa Krismasi lakini pia kote katika mwaka mzima. Je, inawezekana kuwa wewe au watu unaowapenda wanamkosa?

Andiko

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

The Hope Of Christmas

Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.

More

Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa