Tumaini la KrismasiMfano
Jitahidi Kumjua Muumba Wako
Soma mistari ya leo.
Wakati huu wa mwaka, wote tuna kazi za muhimu za kukamilisha. Tuna taarifa za mwisho wa mwaka za kuandika. Tuna kupanga chakula cha sikukuu. Na, bila shaka, tuna zawadi za kununua.
Lakini kuna jambo moja la kuzingatia Krismasi hii: kuanzisha na kukuza uhusiano binafsi na Yesu.
Kwa nini umfahamu Yesu vizuri zaidi? Kuna angalau sababu mbili za muhimu.
Kwanza kabisa, Yesu alikuumba. Biblia inasema, " Kabla chochote hakijakuwepo, Kristo alikuwepo, pamoja na Mungu. Siku zote yuko hai na yeye mwenyewe ni Mungu. Aliumba kila kitu kilichopo-- wala hakuna kilichokuwepo ambacho hakikuumbwa na yeye. Uzima wa milele uko ndani yake, na uzima huu huangaza wanadamu wote" (Yohana 1:1-4).
Una nafasi si tuu ya kukutana na Muumbaji wa mbingu bali kukutana na Muumba wako pia. Umewasikia watu wakisema, " Unapokuwa na mashaka, angalia kitabu cha maelezo." Kumjua Yesu ni bora zaidi. Ukitaka kujua jinsi ya kufaidi maisha, kwa nini usimfahamu yeye aliyekuumba?
Kitu cha pili, Yesu hufungua moyo wako kufurahia maisha ya kusudi, amani, na nguvu. Uhusiano wako na Yesu hutunza sehemu yako mbinguni, lakini hufanya zaidi ya hilo. Mungu anaahidi maisha yenye kusudi, amani, na nguvu kwa wote wanaomjua yeye.
Kumjua Yesu binafsi hubadilisha kila kitu kuhusu jinsi unavyoishi. Kusudi, nguvu, na amani ni mwanzo tuu wa kile Mungu anachotaka kukupa katika maisha.
Bahati mbaya, watu wengi wanaishi katika njia ndogo na isiyojulikana kwa sababu wamejaza maisha yao shughuli zisizo na maana.
Krismasi inapokaribia mwaka huu, fikiria mfanyakazi wa nyumba ya wageni ambaye hakumpa Yesu chumba siku ya Krismasi ya kwanza. Matendo yake hayakumzuia Yesu kuzaliwa. Kitendo chake hakikuzuia kusudi la Mungu katika historia. Ilimuumiza tuu mfanyakazi wa nyumba ya wageni. Alikosa upendeleo wa kumpa mwana wa Mungu malazi wakati wa kuzaliwa kwake.
Ndivyo ilivyo kwako. Kama hupati muda wa kumjua Yesu, unakosa nafasi kumjua Muumba. Unakosa nafasi ya kuwa na kusudi, amani, na nguvu ambayo inatoka tuu kupitia mwana wa Mungu. Unakosa kusudi lake kwenye maisha yako kama humpi chumba.

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.
More
Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa