Tumaini la KrismasiMfano
Maana ya Kupotea
Soma mistari ya leo.
Kama huelewi kusudi la Krismasi, unaweza pia kuacha kupamba na kuweka taa za Krismasi mwaka huu. Unaweza pia kutokununua zawadi za Krismasi. Usifikirie pia chakula cha jioni cha Krismasi.
Kama hujui kwa nini tunasherehekea Krismasi, shamrashamra zote hazina maana.
Kupata maana ya Krismasi, lazima uende mbali zaidi ya hori la kulia ng'ombe, mamajusi, na wachungaji. Yesu alituambia zababu za yeye kuja duniani Krismasi ya kwanza: “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” (LK. 19:10 SUV)
Ni rahisi tuu, Yesu alikuja kwa sababu watu bila Mungu wamepotea. Kupotea kiroho maana yake ni kutengwa na Mungu, kukosa mawasiliano. Pasipo Yesu, kila mtu duniani amepotea--pasipo kujali nguvu, utajiri, au umaarufu walionao.
Na kupotea kwetu kuna kutawanyika kwingi katika maisha yetu. Kujua kwa nini Yesu alikuja duniani, lazima tuelewe maana ya kupotea. Pasipo Mungu, tumepotea.
• Mwelekeo wetu. Lazima tutakuwa na ufahamu mdogo wa tuende wapi na tufanye nini katika maisha yetu.
• ulinzi wake. Tunakuwa wenyewe tunapokuwa hatuko katika ulinzi wa Bwana. Hii ni sababu kubwa watu wamesongwa sana. Wanajaribu kuishi kwa kujiangalia na kujilinda wenyewe badala ya Mungu..
• Uwezo wetu. Hatuwezi kuelewa hata nusu ya vipaji na vipawa tulivyonavyo kama hatuko kwenye uhusiano naye.
• Furaha yetu. Tunaweza kuwa na fedha zote na nguvu zote duniani, lakini bila Mungu hatuwezi kuwa na furaha ya kweli.
• Makao yetu Mbinguni. Mungu anaturuhusu kuasi tukiwa hapa duniani, lakini hakuna uasi mbinguni.
Lakini hakuna aliyepotea na kupoteza thamani yake kwa Mungu. Hata kama huna uhusiano naye, una thamani kubwa kwa Mungu.Kupotea kuna maanisha thamani.Chochote mtu yuko tayari kutumia ili kupata kitu fulani kilichopotea kinaonesha thamani ya kitu kile.
Katika mstari maarufu katika Biblia, Yesu alisema waziwazi thamani yetu: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (YN. 3:16 SUV)
Habari njema ni Mungu alitupenda upeo kamtuma mwanawe duniani katika Krismasi ya kwanza kututafuta na kutuokoa. Hiyo ndiyo sababu ya kusherehekea!

Kuhusu Mpango huu
Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.
More
Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa