Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tumaini la KrismasiMfano

The Hope Of Christmas

SIKU 8 YA 10

Chagua Maisha Bora

Soma mistari ya leo.

Nilipokuwa mtoto mama yangu alinilisha SpaghettiOs. Nilifikiria ni chakula bora ambacho hakijawahi kutokea! Ndipo nikagundua In-N-Out burgers. Ndipo nikatoka kwenye maisha mazuri kwenda maisha bora. SpaghettiOs zilikuwa nzuri, lakini michuzi ya In-N-Out burger ni bora zaidi.

Unaweza kufikiria una maisha mazuri sasa, lakini kama ungeweza kuwa na maisha bora, usingependa kujua habari zake?

Kwa bahati mbaya, kinachotuzuia kuyashika hayo maisha bora ni tabia yetu ya kujiona tumetosheka. Tunadhani tuna kila kitu tunachohitaji.

Zaburi 10:4 Inasema hivi: “Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Hatapatiliza. Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu;”
(‭SUV‬‬).

Kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wa nyumba za kulala wageni katika habari ya Krismasi ya kwanza ( Luka 2), hatuamini tunahitaji wageni zaidi. Tunadhani tuna kila kitu tunachohitaji.

Kuna tatizo moja kwenye kiburi cha namna hiyo: unakosa sababu halisi ya Mungu kukuumba. Mungu alikuumba ili uwe na ushirika naye. Hutaweza kutimiza kusudi lake katika maisha yako, ambalo ni kubwa sana na lenye kuonekana kuliko unavyoweza kufikiria, mpaka umeunganishwa na Mungu, asili ya nguvu ya kweli.

Lakini habari njema ni kwamba hujachelewa. Unaweza kuwa na uhusiano naye pasipokujali yaliyotokea zamani, pasipokujali umemkataa mara ngapi huko nyuma.

Mungu alirahisisha sana ili kila mtu aelewe. Ni maneno mawili tu: mkaribishe ndani.

Yesu alisema, “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”(‭‭UFU.‬ ‭3:20‬ ‭SUV‬‬)

Yesu anabisha mlangoni kwako. Pokea maisha mapya kwa kumruhusu katika maisha yako. Mfanye mkuu wa maisha yako.

Itabadilisha kila kitu.
siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

The Hope Of Christmas

Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.

More

Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa