Tumaini la KrismasiMfano
Usiwe Mbali na Yesu Krismasi Hii
Soma Luka 10:41-42.
Wewe na mimi tunapenda kuyasonga maisha yetu na vitu vingi. Tunajaza sana, tunatumia fedha sana, tunakadiria zaidi, na mara nyingi tunazunguka sana na kujichosha. Matokeo yake, ukweli wa Mungu haupati nafasi ya kustawisha maisha yetu.
Mara nyingi Mungu hukufundisha punje ya ukweli--yawezekana kupitia masomo ya asubuhi ya Biblia au mahubiri ya jumapili-- na unafikiria unahitaji kufanya kitu juu ya hilo, lakini ghafla inazungukwa katika maisha yako na inasahaulika.
Ukweli hauzungukwi katika maisha yako kwa sababu ya uovu. Mara nyingi, mambo mazuri katika maisha yetu huuficha ukweli ambao Mungu anataka kuupanda ndani yetu. Ili kutimiza hatima ya Mungu kwa maisha yako, yawezekana usifanye zaidi; unatakiwa kufanya kidogo.
Chukua mfano wa marafiki wa Yesu Mariamu na Martha. Siku moja walimwalika Yesu kwa chakula cha jioni. Mariamu alitumia muda mwingi jioni ile kumsikiliza Yesu. Martha, kwa upande mwingine, alikuwa anajishughulisha kuhudumia na kuhakikisha kwamba kila kitu kiko vizuri.
Martha alikasirika kwa sababu alikuwa anashughulika peke yake wakati dada yake amekaa tuu na Yesu. Ndipo Yesu alipomwambia: " Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.” (LK. 10:41-42 SUV)
Maisha yako yanapofika mwisho, jambo moja tuu litakuwa la muhimu: je, ulimfahamu mwana wa Mungu? Zawadi zaidi za Krismasi ulizoweza kununua kwa sababu ya masaa mengi kukaa ofisini hakujalishi. Muda wote unaotumia kuandaa chakula kizuri cha likizo hakujalishi pia. Lakini iwe ulitumia muda mwingi kumfahamu Yesu ni muhimu sana kwa miaka mingi ijayo.
Kwa hiyo furahia wakati wa Krismasi. Funga zawadi. Tayarisha nyumba yako kwa sherehe. Weka kumbukumbu na familia. Lakini usiache Krismasi hii ikupite pasipo kuwa na muda miguuni pa Yesu. Baada ya kila kitu kupita katika Krismasi, kumwabudu Yesu ndiyo kitu pekee kitakachodumu.

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.
More
Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa