Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tumaini la KrismasiMfano

The Hope Of Christmas

SIKU 2 YA 10

Safari ya Kumjua Yesu ina thamana kuu

Soma Mathayo 2:1.

Kuutafuta ukweli sio kazi ya wakati wakati. Inaichukua juhudi yako yote. Mamajusi wanatufundisha hii ndio hadithi kamili ya Krismasi.

Mamajusi walikuwa tayari kwenda urefu wowote ule ili kuupata ukweli. Mathayo 2:1 inasema, "Wakati Yesu alipozaliwa Mamajusi kutoka Mashariki walikuja Yerusalemu"(NCV). Tunaweza waza kwamba Mamajusi walisafiri maili nyingi kutoka Mashariki ya Mbali hadi Mashariki ya Kati kwa gharama ya juu ili kumpata Yesu.

Yesu alizaliwa Bethlehemu, ambayo ni maili sita tu kutoka Yerusalemu. Wakati wa kuzaliwa kwake Yesu, Yerusalemu ilikuwa kituo cha kiroho ulimwenguni. Kila aina ya shughuli za kiroho zilifanyika Yerusalemu. Viongozi wote wakubwa wa kidini duniani walikuwa Yerusalemu, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwa akimtafuta Yesu. Ni watu wa nje pekee — Mamajusi kutoka tamaduni tofauti — waliokuwa wanamtafuta Yesu.

Mfalme Herode alimkosa mtoto Yesu. Vilevile wafanya biashara wa Bethlehemu. Wewe pia, waweza kuwa na Yesu hapo ulipo na bado umkose ikiwa humtafuti.

Lakini Mamajusi walimtafuta Yesu. Walikuwa tayari kusafiri kwa miezi minne au mitano chini ya jua kali la jangwani ilimradi wampate Yesu. Walilichukulia swala la kumtafuta Mungu kwa uzito. Walikuwa tayari kufanya lolote kumpata.

Hiyo ni hekima Tunahitaji kufanya vivyo hivyo. Hatuwezi kubali vizuizi vyovyote vile kutuzuia kumtafuta Mungu. Hayo ndiyo mafanikio ya muhumi zaidi ulimwenguni.

Yesu alisema kwamba ufalme wa Mbinguni ni kama lulu ya thamani luu, kwa hivyo tutauza kila kitu tulichonacho kupata hiyo lulu. Ni kama Mamajusi kutoka Mashariki waliyafahamu haya hata kabla ya Yesu kuzungumzia mfano huo.

Mamajusi walikuwa tayari kufanya lolote ilimradi wamuabudu Yesu. Walikuwa tayari kuacha makaazi yao ya faraja kwa ajili ya safari ndefu na ngumu kwa sababu walikuwa na nia njema katika kumtafuta Yesu. Walitaka kumuabudu.

Ni kitu gani uko tayari kukiacha ili kumuabudu Yesu?

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

The Hope Of Christmas

Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.

More

Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa