Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Mwaka mmoja kamili baada ya wana wa Israeli kuondoka Misri, Musa aliweza kuisimamisha hema ya kukutania. Kazi yote ilikuwa imegawiwa kwa watu kwa kufuata ujuzi na vipawa vyao walivyopewa na Mungu. Kwa pamoja walikuwa wametekeleza maagizo yote anayoyaagiza Mungu na kutimiza malengo ya huduma. Huleta baraka. Humfanya Musa, kiongozi wao, kumshukuru Mungu kwa wote waliochangia na kuwaombea heri.Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama Bwana alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo; basi Musa akawaombea heri(m.43). Wewe uliyepewa kazi, fanya sawasawa na kwa wakati wake, ukiga mfano huo; na Mungu akubariki.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More