Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Mtunzi wa Zaburi hii anaendelea kuelezea heshima na utukufu wa mfalme huyu akihusianisha na fahari na mapambo ya sherehe ya arusi. Kisha anatoa angalizo kwa malkia mpya (bibi arusi) kwamba asahau maisha ya nyuma na kuwa mwaminifu kwa mumewe. Picha hii inahusu Yesu na Kanisa. Hivyo Kanisa, yaani mimi na wewe tulioposwa na Yesu Kristo, tunapaswa tubadilishe tabia zetu na kuwa waaminifu wa Yesu (Bwana Arusi).Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. Na binti Tiro analeta kipawa chake, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako(m.10-12). Kumbuka pia jinsi Yohana anavyoeleza katika Ufu 19:6-8:Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Tumngojee Bwana Yesu. Anakaribia!
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More