Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Jambo kuu hapa ni kwambatunayeKuhani Mkuu anayetosheleza haja zetu. Tuna uhakika kwa sababu Yesu ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi mbinguni. Ni mhudumu wa patakatifu, yaani mbinguni kwa Mungu. Agano la kale lililofanyika mlima Sinai ni kivuli cha agano jipya la Yesu Kristo. Vivyo hivyo ukuhani wa agano la kale ni kivuli cha ukuhani wa kweli aliotoa Yesu. Yeye hutuombea kwa Mungu moja kwa moja. Wale wanaomwamini na kumfuata, japo wako duniani, kwao ni mbinguni aliko Kuhani wao.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More