YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

DAY 6 OF 31

Yesu alipokufa msalabani alikuwa sadaka bora kuliko ile ya wanyama iliyotolewa na makuhani. Sadaka ya Yesu ilikubalika kwa sababu yeye ndiye mwakilishi mkamilifu ambaye hakutenda dhambi. Upatanisho alioufanya ni wa kudumu, kwa sababu Yesualiingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu(m.24).Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini(Mt 27:51). Kupasuka kwa pazia la hekalu hapa duniani kunaashiria uwazi na uhakika wa kwenda mbele za Mungu na kupata msamaha wa dhambi. Sasa tunaweza kukaribia kiti cha neema cha Mungu bila mtu wa kati, jambo tunalohimizwa kufanya katika Ebr 4:16: Tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Day 5Day 7

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More