YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

DAY 9 OF 31

Kuna tofauti kubwa kati ya dhabihu zilizotolewa na makuhani na ile moja aliyoitoa Kristo. Makuhani walitoa dhabihu mara nyingi, kwani hazikuweza kufuta kumbukumbu. Kila mara iliwabidi kujiandaa kwa toleo lingine. Yesu, baada ya kutoa sadaka ya nafsi yake,aliketi mkono wa kuume wa Mungu(m.12). Kuketi kwake huashiria mapumziko baada ya kukamilisha kazi, tena ushindi na utawala. Yesu ana mamlaka ya kutusamehe. Hapana haja ya toleo lingine, kwa sababu imeandikwa kuwa kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa(m. 14). Tafakari kwa utulivu maana yake kwako.

Day 8Day 10

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More