YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

DAY 13 OF 31

Ni nini kinachofuata baada ya kufanya agano na Mungu? Ni kuishi naye sawasawa na agano hilo linavyosema. Yametajwa mambo matatu: Kupokea maagizo ya Mungu, kuiheshimu siku yake ya kupumzika, na kumtolea shukrani. Kuishi hivyo ni kumtumikia Mungu. Mungu ametupa siku 6 za kushiriki uendelezaji wa uumbaji wake kwa kufanya kazi. Kisha siku ya saba ni ya kusherehekea matunda ya kazi pamoja na Mungu. Kumbuka kuwa Bwana wa pumziko lako ni Kristo:Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato(Mt 12:8). Kuhusu kutoa sadaka, tafakari ilivvyoandikwa katika m.5:Katwaeni kati yenu matoleo kwa Bwana; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba.

Day 12Day 14

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More