Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Musa aliongoza ujenzi wa hema ya kukutania akisaidiwa na watu wengi wenye ujuzi maalumu. Jumuia nzima inashiriki, huduma ya kila mtu inategemeana na ya mwenzake. Taarifa katika somo hili pamoja na Kut 36:9-38:20 huthibitisha uangalifu na uaminifu wa kila aliyechangia katika ujenzi. Wote walioitwa na kupewa wajibu wa kuongoza wengine, wajifunze kugundua na kutumia vipawa au karama za wale wanaowaongoza. Mwombe Mungu akupe kutambua karama au kipawa chako, kisha umruhusu Kristo akitumie atakavyo.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More