Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Baada ya hema ya kukutania kuwekwa wakfu, Mungu aliingia ndani yake, utukufu wake ukiijaa. Hivyo Mungu alipata kukaa kati ya watu wake na kuwaongoza katika safari zao zote. Baadaye hekalu lilipojengwa nalo likajaa utukufu wa Mungu.Wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana(2 Nya 5:13-14). Lakini Waisraeli, yaani taifa la agano, walipokengeuka na kuacha kumfuata, utukufu wa Mungu uliondoka. Mwisho hekalu likabomolewa kabisa. Zingatia mambo hayo ya kihistoria kwa kuyalinganisha na habari ya hekalu la Mungu siku hizi, ambalo ni sawa na waumini wote:Mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi(1 Kor 3:16-17).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More