Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Musa alimaliza ujenzi wa hema ya kukutania kwa kuisimamisha na kuwakabidhi makuhani kuitunza. Kila kifaa kilicho ndani yake ni cha muhimu. Leo nyumba ya Mungu ni Kanisa. Katika agano jipya la Kristo Yesu ametutengenezea njia iliyo hai, iendayo moja kwa moja kwa Mungu, ili tuweze kufika mbele yake wakati wowote kwa maombi yetu. Kwa hiyo, kwa sasa sisi hatupategemei mahali patakatifu, bali sisi sote tulioitwa na Mungu na kumwamini Yesu ndio Kanisa lake Mungu. Tafakari hali yetu hiyo ilivyofafanuliwa katika 1 Kor 3:16-17 na 6:19-20:Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. ...Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More