YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

DAY 19 OF 31

Mungu hawaiti watu kwa huduma yake bila kuwatambulisha kwa wale watakaohudumiwa. Alikuwa amekabidhi kazi ya huduma ya ukuhani kwa kabila la Walawi, na nyumba ya Haruni inatokana na Walawi. Kwa hiyo Haruni na wana wake ndio wanaowekwa wakfu kwa wito huo maalumu. Tangu Yesu alipokuja kuwa Kuhani mkuu, huduma hii maalumu ya ukuhani haipo tena, isipokuwawotewamwaminio Yesu wamekabidhiwa ukuhani wa kifalme wa kutangaza au kushuhudia matendo makuu ya wokovu wa Mungu.Kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. ... Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu (1 Pet 2:5 na 9).

Day 18Day 20

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More