Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Zaburi hii inamsifia mtu mmoja ambaye si wa kawaida. Wakati unaposoma zaburi hii jiulize maswali kadhaa: Ni nani ambaye ni mzuri sana kuliko mwanadamu, ambaye neema imemiminwa midomoni mwake? Ni nani ambaye ameipenda haki na kuichukia dhuluma, ambaye Mungu amempaka mafuta, mafuta ya furaha kuliko wenzake? Ukiichunguza zaburi hii kiroho, utagundua kuwa picha hii inamhusu Yesu na Kanisa lake. Yesu Kristo ndiye mtu pekee aliyeishi duniani akiwa katika hali zote za kibinadamu lakini hakutenda dhambi.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More