Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Yeroboamu II alitawala Israeli miaka 41 baada ya baba yake kufariki. Alifanya maovu machoni kwa BWANA akiendeleza ibada za miungu alizoanzisha Yeroboamu I wa Israeli. Kuhusu Yeroboamu II imeandikwa kwambaakafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; wala hakuyaacha makosa yote ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli(m.24).Linganisha habari hiyo na ilivyoandikwa kuhusu Yeroboamu I katika 1 Fal 12:28-31:Mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. Tena akafanya nyumba za mahali pa juu, akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani. Angalia kuwa maovu hayo aliyofanya mfalme, hayakumzuia Mungu asione taabu ya watu wake waliokaa katika sehemu za nchi zilizotekwa. Anapokosekana mkombozi wa kumsaidia, Mungu anamtumia Yeroboam II:Bwana hakusema ya kwamba atalifuta jina la Israeli litoke chini ya mbingu; lakini akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi(m.27). Tujifunze kuwa huruma ya Mungu haizuiliki. Aweza kumtumia yeyote anapotaka kuwaokoa watu wake.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More