Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Mfalme Amazia alituma ujumbe wa kivita kwa Mfalme Yehoashi wa Israeli, ingawa Waisraeli na Wayuda ni ndugu. Jibu la Yehoashi laonyesha kosa la Amazia: Ana kiburi kutokana na ushindi aliopata dhidi ya Waedomi. Ila Amazia hakusikiliza onyo, alikuwa na shingo ngumu. Na kwenye vita Amazia na watu wa Yuda walitekwa, ukuta wa Yerusalemu ulivunjwa, na nyara nyingi zilichukuliwa kwenye nyumba ya BWANA. Mwisho Amazia aliuawa. Ni mfano haiunaotuonya kwamba kiburi hutangulia anguko(Mit 16:18).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More