Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Mungu anapotaka kazi yake itendeke kwa utaratibu, ustadi na utakatifu wake, huandaa mazingira na kazi yenyewe. Kisha anawaandaa watu maalumu wa kuifanya huduma hiyo. Kwanza anawaita, kisha, wanapopokea wajibu wao wa kazi, anawajaza hekima, akili, ujuzi na ufahamu unaohitajika kwa kazi inayohusika.Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezalelimwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina(Kut 31:1-3). Mbele ya Mungu hakuna maarifa ama ujuzi unaokosekana. Je, Mungu amekuita kujenga ufalme wake? Basi uitikie kwa ujasiri ukitegemea kwamba atakupa pia zile karama zinazohitajika.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More