Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample
Msingi wa huduma ya Yesu Kristo ni kuwa mjumbe wa agano jipya kwa kutoa nafsi yake kuwa fidia ya dhambi. Dhambi ilikuwa kizuizi kati ya mwanadamu na Mungu, lakini kwa kujitoa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu, Yesu amekuwa kipatanishi chetu na Mungu, na kizuizi hicho hakipo tena. Tunaposhiriki sakramenti ya meza takatifu, tunapokea kipawa hiki cha ondoleo la dhambi. Anayekipokea kwa imani ana uhakika wa msamaha wa dhambi zake. Hii pia ni ahadi ya kweli ya kupata kurithi uzima wa milele.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More