YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

DAY 4 OF 31

Katika Agano la Kale kuhani mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja kila mwaka kutoa dhabihu ya dhambi. Kristo alipokuja yeye alijitoa mara moja kuwa sadaka itoshayo siku zote. Kwa hiyo kupata msamaha wa dhambi hakuhitaji tena sadaka. Kila mmoja anaweza kuomba msamaha moja kwa moja kwa Mungu. Iamini damu ya Yesu iliyotolewa msalabani kuleta ukombozi. Imepokelewa mbinguni, tunaambiwa katika m.12:Kwa damu yake mwenyewe [Yesu] aliingia mara moja tu katika Patakatifu [pa mbinguni], akiisha kupata ukombozi wa milele.Hata duniani ina matokeo yake makubwa. Tunapomwamini Yesu, inasafisha dhamiri zetu na matendo mafu tupate kumwabudu Mungu aliye hai.

Day 3Day 5

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More