Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 20 YA 31

Waisraeli ambao Nebukadreza aliwachukua mateka wanarudi Yerusalemu. Kurudi kwao ni kukamilifu, maana walirudikila mtu mjini kwake(m.1). Je, kuna dhambi iliyokuteka katika maisha yako? Ukitubu, Mungu atakurejesha kwake kwa ukamilifu, maana Mungu hutenda kazi yake kwa ukamilifu.Wakuu wa mbari za baba zao, hapo walipoifikilia nyumba ya Bwana, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu sitini na moja elfu ,na nane za fedha elfu tano,na mavazi mia ya makuhani(m.68-69). Je, umemtolea Mungu shukrani zako katika mambo gani aliyokutendea?

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz