Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Ujenzi wa nyumba ya Bwana ulifanywa kwa ushirikiano wa watu na ustadi ukizingatia mgawanyo wa kazi. Jukumu la kusimamia kazi ya ujenzi lilitekelezwa na vijana wa umri wa miaka ishirini na kwenda juu. Ilikuwa kazi ya Walawi kusimamia watenda kazi.Zerubabelina viongozi wenginewakawaweka Walawi, hao wenye miaka ishirini na waliozidi, ili kuisimamia kazi ya nyumba ya Bwana(m.8-9). Je, unapotenda kazi ya Bwana unafanya matayarisho ya kutosha na usimamizi thabiti, au unaacha tu ukisema Mungu mwenyewe atajua? Pia wakati wa kuanza kazi walimtukuza Mungu. Walifanya hivyo wakiwa na imani kuwa kazi wanayoanza ni ya Bwana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz