Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Pamoja na amri ya Mfalme Artashasta ya kuwataka wana wa Yuda kusimamisha ujenzi wa nyumba ya Bwana, ujenzi huo unaendelea chini ya uongozi wa Mungu mwenyewe kupitia manabii Hagai na Zekaria. Hawawaliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli. Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia(m.1-2). Liwali Tetani alipojaribu kusimamisha ujenzi,lakini jicho la Mungu lilikuwa likiwaelekea wazee wa Wayahudi, hao wasiwazuie,wana wa Yuda wakaendelea na kazi (m.3-5). Baada ya kushindwa kuwazuia, Liwali anamwandikia Mfalme Dario kumwarifu juu ya ukaidi wa wana wa Yuda. Tumeamriwa kutii mamlaka iliyo juu yetu (kwa ufahamu zaidi, soma mwenyewe Rum 13:1-7). Lakini amri hiyo, maana yake siyo kutii amri zinazopinga amri za Mungu au maadili ya Kikristo. Tafakari walivyofanya wazalisha wa Waebrania kule Misri:Mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni ... Lakini wala wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifahdi hai wale wanaume(Kut 1:15-17).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz