Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Kabla ya kurudi Yerusalemu Ezra anawakabidhi Waisraeli mali zote zinazotakiwa kupelekwa Yerusalemu ikiwa ni fedha na dhahabu na vitu vingine vya thamani. Kila mmoja anapewa kipimo fulani ambacho kitapimwa tena wakifika Yerusalemu. Licha ya kwamba Ezra anawaamini watu hawa, bado anawakumbusha kuwa wao pamoja na mali hizo za Mungu ni watakatifu. Tunaona kuwa inafaa mali za Mungu zithaminiwe na kutunzwa vizuri kwa uaminifu. Ndiyo maana kanisani tunafanya ukaguzi wa fedha na mali nyingine kila mwaka.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz