Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Ezra anaarifiwa kuwa Waisraeli waliorudi Yerusalemu kutoka uhamishoni wameanza kuoana na watu wa mataifa mengine kinyume na agizo la Mungu kwa Waisraeli wakati wa kuingia nchi ya ahadi kuimiliki. Hapo waliambiwa kuhusu wenyeji:Uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine(Kum 7:1-5). Hapa tunaona kuwa kabla ya kuoa au kuolewa lazima utafakari sana kama uoe au kuolewa na mtu asiye Mkristo. Katika sala yake, kwanza Ezra anamsifu Mungu na haki yake kwa kukiri watu wake walivyomkosea:Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo(m.7). Kisha anatoa shukrani zake kwa Mungu:Tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu(m.8). Hivyo anaweza kumwomba Mungu awasamahe:Ee Bwana, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili(m.15). Sisi tukimjongea Mungu kwa maombi tufanye sala tukikumbuka hayo yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz