Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Upo msemo wa Kiswahili usemao, “Leo ni leo, asemaye kesho ni muongo”. Mungu hutoa zawadi ya kuishi tukiamka kitandani na kuona siku nyingine mpya imeanza. Kila siku anatutayarishia matendo mema tuyatende. Usingoje kesho, hujui itakuwaje kwako. Hali kadhalika tusipange siku zijazo kana kwamba tunaweza kuziamua sisi wenyewe, bali tujitoe kwa mapenzi ya Mungu, tukimwomba atulinde dhidi ya kiburi, na atupe neema, nia na ujasiri wa kuyatenda. Huu ndio uzima wetu tulio nao kila siku katika Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz