Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu(m.1). ”Injili” maana yake ni "habari njema". Kuja kwa Yesu Kristo kulikuwampango wa Mungu tangu awali. Kwa hiyo manabii wa A/K walitabiri juu ya jambo hili, kwa mfanokama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayeitengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake(m.2-3). Fikiria jinsi inavyokuwa Rais anapotangaza kuzuru mahali fulani. Maandalio ya kumpokea ni mengi, barabara zinatengenezwa n.k. Kabla Yesu Kristo mwenyewe hajaja alitangulia mtu wa kumtengenezea njia. Yohana Mbatizaji alikuwa chombo kiteule cha Mungu cha kuwaandaa watu kiroho.Alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao(m.4-5).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz