Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Hata alfajiri na mapema sana[Yesu]akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko(m.35). Katika utumishi wake, Yesu alitumia muda mwingi kwa ajili ya maombi. Mtu mmoja amesema hivi: "Kama Yesu, Mwana wa Mungu, alihitaji sana kuomba ili kuweza kutenda kazi yake sawasawa, sisi Wakristo, je?" Yesu alikuwamaskini wa roho(Mt 5:3). Yaani Roho Mtakatifu alimfanya Yesu atambue kuwa anamhitaji sana Mungu Baba katika kila jambo la maisha yake!Heri walio maskini wa roho!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz