Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 11 YA 31

Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake(m.7). Habari za Yesu zilipozidi kuenea, umati wa watu ulimfuata. Kwa hiyo ikabidi wakati fulani Yesu na wanafunzi wake wapate kukaa peke yao ili wapumzike na ili Yesu apate kuwafundisha. Umati ulipozidi, Yesu akawachagua mitume 12 kati ya wanafunzi wake ili wamsaidie katika kazi yake. Neno muhimu la kuzingatia ni kwamba wajibu wakwanzawa mtumishi wa Bwana si kuhubiri wala kutoa pepo, bali nikuwa pamoja nayeYesu (m.14). Huu ndio msingi wa utumishi. Kwa hiyo Yesu anasisitiza:Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu!(Yn 15:4-8).

Andiko

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz