Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 12 YA 31

Waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema,[Yesu]ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo(m.22). Mji wa Yerusalemu ulikuwa makao makuu ya dini ya Kiyahudi.Waandishiwalikuwa ni "wanatheolojia". Msimamo wao ulikuwa katika mapokeo ya wazee. Yesu aliyakataa mapokeo haya akisema si mafafanuzi sahihi ya torati (= sheria ya Musa). Kwa hiyo waandishi walidai kuwa Yesu ni mwongo anayemkufuru Mungu, maana alijidai kuwa na amri ya kimungu. Hiyo ilionekana hasa aliposamehe dhambi. Kwa mfano tunasoma katika 2:5-7 kwambaYesu alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?Ila Yesu aliwaonya kuwa wakizidi kuifanya migumu mioyo yao watamkufuru Roho Mtakatifu:Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele, kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu(m.28-30).

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz