Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 01/2025](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F54349%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?(m.41).Jibu lake:Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika(Yn 1:3).Yesu niMwana wa Mungu(Mk 1:1). Pamoja na Mungu aliziumba mbingu na nchi. Hakuna jambo lisilowezekana kwake. Hata Tanzania mara kwa mara tumeuona ukuu wake. Kwa mfano kwenye mikutano ya hadhara aliposikia maombi yetu ya kupata hali nzuri ya hewa. Tusiwe waoga tukiwa taabuni. Mwana wa Mungu yu pamoja nasikilasiku, kama alivyokuwa pamoja na wanafunzi wa kwanza baada ya kuchukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu.Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo(Mk 16:19-20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 01/2025](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F54349%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz