Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Wakajikwaa kwakeYesu (m.3). Yesu alikuwa amefikampaka nchi ya kwao, yaani nyumbani Nazareti(m.1). Watu wa nyumbani walikuwa wanashangaa. Kwa upande mmoja walikubali kuwa mafundisho yake na matendo yake ni ya pekee sana.Ilipokuwa sabato, [Yesu] alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?(m.2). Kwa upande mwingine walijua ni seremala tu wala si mwalimu wa dini (mwanatheolojia) aliyepitia mafunzo kwa walimu wao wa dini ya Kiyahudi.Huyu [Yesu] si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake(m.3). Huenda walifikiri anayafanya kwa nguvu ya Shetani? Neno la Yesu katika m.4 kuhusu nabii kutokukosaheshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake, lituonye: Tusijikwae, Mungu akiamua kumjalia mtu wa kwetu kwa njia ya pekee!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz