Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 19 YA 31

Nabii Yeremia alikuwa ametabiri kuwa Waisraeli watakuwa uhamishoni Babeli kwa muda wa miaka sabini. Koreshi, mfalme wa Uajemi, anapotoa amri kwa Waisraeli kurudi kwao, ni Mungu mwenyewe anayeiamsha roho yake kutoa hiyo amri. Koreshi anawatangazia Waisraeli baraka alizopata kutoka kwa Mungu, na pia kwamba ataka wamjengee nyumba katika Yerusalemu. Mara tu baada ya kutoka kwa amri hiyo, maandalizi yanaanza kwa ajili ya utekelezaji. Je, wamkiri Bwana kuwa ndiye akuwezeshaye katika mafanikio yako?

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz