Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Ujenzi wa nyumba ya Bwana unaanza kupata upinzani. Maadui wa Yuda na Benjamin wanaomba kushiriki katika ujenzi wa nyumba ya Bwana: Wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa(m.2). Lakini walikataliwa kwa sababu Yuda walisema watu wa Mungu tu ndio walioamriwa kujenga na Mfalme Koreshi. Hapa tunaona viongozi wa watu wa Yuda wakiwa namsimamo. Kwa kutaka urahisi katika kutenda kazi ya Bwana tunaweza kuiharibu. Je, ni mara ngapi katika makanisa yetu tumefanya harambee na kualika watu ambao sio Wakristo ili mradi tu tupate fedha?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz