Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
Mfalme Dario anafanya utafiti wa nyaraka za kale na kugundua kuwa Mfalme Koreshi alikuwa ametoa maagizo ya kujengwa kwa nyumba ya Mungu Yerusalemu. Bila kusita Mfalme Dario anaamuru ujenzi wa nyumba ya Mungu uendelee bila kipingamizi: Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na hao wenzi wenu wa Kiajemi, mlio ng'ambo ya Mto, jitengeni na mahali pale; iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake(m.6-7). Baada ya hapo ujenzi unamalizika. Lakini tafakari pia ilivyoandikwa katika m.14:Wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli .... Ndipowakaiweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha ... na wakawaweka makuhani katika kura zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; vile vile kama vilivyoandikwa katika chuo cha Musa. Kisha, wana wa uhamisho wakaifanya Pasaka ... wakaifanya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa furaha, kwa muda wa siku saba; kwa kuwa Bwana amewafurahisha(m.16-22). Hapa tunaona kwamba kazi ya Mungu haiwezi kuzuiwa na mwanadamu. Kukitokea dalili za upinzani katika kutenda kazi ya Bwana tunatakiwa kutokata tamaa, bali tuzidi kuomba.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz