Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 17 YA 31

Hapa twajifunza kwamba ombi la mtu si kitu kidogo kwa Yesu. Yesu aliguswa na taabu ya mtu yule, akaamua kwenda kumsaidia. Ndugu msomaji, tusikawie kumkabidhi Yesu taabu zetu tukimwomba na kumsihi atusaidie! Ila wakati mwingine inaonekana kana kwamba Yesu amechelewa kutujibu. Ndipo tunajiuliza: Je, hajatusikia au ametusahau? Ndivyo ilivyokuwa siku hiyo. Yule binti akafa kabla Yesu hajaja.Wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu?(m.35) Ila angalia jibu la Yesu:Usiogope, amini tu!(m.36). Hii itutie moyo kumtwika fadhaa zetu zote.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz