Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 01/2025](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F54349%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu(m.11). Yesu alitumia sana mifano alipowaeleza watu juu ya ufalme wa Mungu: [Yesu]akawafundisha mambo mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake(m.2). Hivyo aliiweka wazi habari ya ufalme wa Mungu, haikuwa tena siri. Hata hivyo kuna wengine waliokuwa hawaelewi. Ila wanafunzi wa Yesu walitambua, maana walipokea kwaimani(m.20). Ndivyo ilivyo hata leo! Fundisho:1.Neno la Yesu lipewe umuhimu wa kwanza kwa maisha yetu yote.2.Tumsihi Yesu atufunulie maana ya neno lake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Wanafunzi ni kielelezo kizuri: [Yesu]alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza habari za ile mifano(m.10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 01/2025](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F54349%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz