Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 10 YA 31

Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza(m.4).Sabatokwa Wayahudi ni kama Jumapili ilivyo kwetu, yaani, siku ya kumwabudu Mungu na siku ya kupumzika. Kama Mwana wa Mungu, Yesu alijua maana ya sabato kuliko mtu mwingine.Ndiye Bwana wa sabato(2:28). Na mafundisho yake ni wazi:Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato(2:27)!Lakini Mafarisayo walifungwa na mapokeo ya wazee hata wasiweze kulifurahia tendo jema. Hali yao hiyo ilimgusa sana Yesu,akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza(m.5-6).

Andiko

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz