Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 7 YA 31

Ikasikiwa ya kwamba [Yesu]yumo nyumbani(m.1). Yesu alipoanza kazi yake rasmi, alitoka Nazareti na kuhamia Kapernaumu. Mathayo ameeleza sababu:Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia(Mt 4:12-16). Sehemu hiyo ya nchi aliyoenda Yesu iliitwa Galilaya. Wayahudi wa sehemu ya Yerusalemu na Uyahudi hawakujali Wayahudi waliokaa Galilaya. Hata hivyo Yesu aliamua kufanya kazi sana katika sehemu hii ya nchi kuliko sehemu nyingine (1:39: [Yesu]akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo! Shabaha kuu ya Yesu ilikuwa kuondoa dhambi. Kwa hiyoalipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako (m.5). Maana uzima wa milele ni muhimu kuliko uzima wa maisha haya.Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu(Mk 8:36-38).

Andiko

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz