Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Kuja kwa Yesu ulimwenguni kulikuwa na shabaha ya kuwaokoa wanadamu waliokuwa katika giza la dhambi. Tupokee wokovu kutoka kwake. Kutokumkubali Kristo ni kuishi gizani. Mamajusi wa Mashariki walipofuata mwongozo wa Mungu kwa usahihi, walimwona Yesu. Tumtafute Yesumaadamu anapatikana, tumwitemaadamu yu karibu(Isa 55:6). Kutamani kutenda dhambi ni kukubali kuishi maisha ya gizani. Uyakatae maisha ya giza, umkubali Yesu aliye uzima wa ulimwengu. Kwetu sisi Yesu ni nuru ya ulimwengu. Natukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote(1 Yoh 1:7). Umpokee leo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz