Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 4 YA 31

Yesu aliwasaidia watu kiroho na kimwili.Kirohoaliwasaidia kwa kufundisha na kuihubiri Habari Njema:Siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi.Kishaakawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea. Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo(m.21-22, 38-39).Kimwilialiwasaidia kwa kuponya magonjwa yao.Walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. ... Akawaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali(m.32, 34).Ni muhimu sana sisi Wakristo kuzingatia kuwa Yesu alitofautisha kati ya wagonjwa wa kawaida na wenye pepo!1.Alimponya mtu mwenye pepo kwa kumkemea:Palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, ... Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka(m.23-27).2.Alimponya mtu mwenye homa ya kawaida:Walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake. [Yesu] akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia(m.29-31). Tusiwatie watu hofu ya kuwa na pepo kama hawana!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz