Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
Swali la Petro lingeweza kuwa swali lako pia! Jambo hili la kumsamehe mtu aliyetukosea linatatiza sana wanadamu na hata Wakristo. Jibu la Yesu ni kwamba kusamehe kwetu kusiwe na mwisho, tena tusamehe kwa moyo.Yesu akamwambia [Petro], Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini(m.22).Fikiria pia Yesu anavyohitimisha mfano wa mtumwa yule asiyetaka kusamehe, bwana wake akampeleka kuadhibiwa mpaka hapo atakapolipa deni lake lote:Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake(m.35). Na zaidi, Yesu anataka wewe uliyekosewa uchukue hatua ya kwanza ya kujaribu kupatanishwa na ndugu yako:Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo(m.15). Yatawezekanaje haya? Mfano wa Yesu utakusaidia. Unahitaji sana kukumbuka na kutambua ukubwa wa deni la dhambi zako ambalo Mungu amekusamehe bure kwa neema yake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz