Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu(m.24). Kwa mazingira ya Wayahudi ngamia alikuwa ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengine, na tundu ya sindano ilikuwa ni tundu dogo kuliko matundu mengine. Kwa Tanzania tungesema tembo badala ya ngamia. Kwa mfano huu Yesu anasisitiza kwamba ni jambo lisilowezekana. Huenda tunashangaa kama wanafunzi tukiuliza,Ni nani basi awezaye kuokoka(m.25)?Jibu:Kwa Mungu yote yawezekana(m.26). Mtume Yohana anafafanua zaidi jinsi Mungu anavyoweza kutuokoa kwa njia ya Yesu Kristo:Wote waliompokea [Yesu] aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu(Yn 1:12-13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz