Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Tusikubali dhambi ijulikanayo kuwepo katika kanisa letu bila kuchukua hatua ya kumsaidia mwenye shida. Wakristo tu mwili wa Kristo, tumeunganishwa pamoja kwa Roho Mtakatifu, tunategemeana. Kwa hiyo hatuwezi kusema "shauri lake" juu ya shida ya Mkristo mwenzetu. Mkono wako ukipata kuumia, hata mwili wako mzima unaumia. Mwili hauna raha, bali utajitahidi sana kuusaidia mkono. Leo Yesu anatupa mwongozo wa namna ya kusaidiana. Huenda mwongozo huu umeandikwa pia katika katiba ya kanisa lako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz