Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Tunaonyeshwa hali njema ya mbingu mpya na nchi mpya atakazoziumba Mungu. Yote yatakuwa mapya. Mwenye kiu ya kuingia hapo, anapewa ahadi mbili: Uzima watolewa bure, kama yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi anavyosema katika m.6:Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Tukiwa tu wana wa Mungu, tutaurithi huo uzima, kama Yesu anavyoendelea kuahidi katika m.7:Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Ila hutakiwa utakatifu na kushinda. Kila anayemwamini Yesu anafanyika mwana mtakatifu wa Mungu, kwani Yesu aliyetufia ni mtakatifu na hututakasa. Tukiishi maisha mapya ndani yake, tunawekwa huru mbali na dhambi, na ni matayarisho ya kuurithi huo uzima. Zingatia jibu alilopata Yohana katika Ufu 7:13-14:Mmoja wa wale wazee aliniambia,Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz