Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

SIKU 22 YA 30

Mwaka wa 14 wa umiliki wa Hezekia, Mfalme wa Ashuru alipigana na miji yote ya Yuda na kuitwaa. Ili kulinda Yerusalemu, Hezekia alijisalimisha akimpa Senakeribu fedha na dhahabu zote katika nyumba ya BWANA.Hezekia aliiondoa dhahabu iliyokuwa juu ya milango ya hekalu la Bwana, na juu ya nguzo, ambazo Hezekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amezitia dhahabu, akampa mfalme wa Ashuru(m.16). Lakini Senakeribu hakuridhika. Alituma ujumbe mzito kwa mfalme Hezekia akidharau imani yake katika Bwana na kusema kwamba Wayuda hawana kimbilio. Lengo lilikuwa kumtisha:Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule amiri, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa hao watu walio ukutani. Lakini yule amiri akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Je! Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?(m.26-27). Hezekia alijibu kwa kunyamaza huku akitegemea neno la Bwana kama lile katika Zaburi 20:Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake; Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama. Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz